WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Thursday, 9 April 2015

UHALIFU MTANDAO NI TISHIO KWA UCHUMI WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Mkutano wa “Connect East Africa” uliofanyika Diani Nchini Kenya umekamilika huku ukibaini yakua Uchumi wanchi za Afrika mashariki umeathiriwa sana na uhalifu mtandao kiasi ambacho mambo matano ya juu yanayo athiri uchumi wa nchi za afrika mashariki ni pamoja na Uhalifu mtandao.

Akitolea Ufafanuzi kauli hiyo Meneja wa PwC bwana. John Kamau alieleza uhalifu mtandao umeendelea kutengeneza vichwa vya habari nabado utaendelea kufanya hivyo kwa muda. Na kwa sasa tayari uhalifu huu umeingia katika mambo makubwa matano yanayo zorotesha ukuaji wa uchumi katika nchi za Afrika Mashariki.

Aliongeza kwa kusema kwa mujibu wa takwimu asilimia 93 ya watu wameonyesha uhalifu mtandao ni moja ya vitu vinavyo takiwa sana kufahamika vizuri huku asilimia 7 ya watu wakionyesha kutojali. Wahalifu mtandao wameendelea kuwa na njia madhubuti na uwezo wa juu kufanikisha uhalifu huu.

Cha kutisha zaidi kwa sasa wahalifu mtandao wameendelea kuunganisha nguvu kwa kuvuka mipaka na kupelekea wahalifu mtandao kutoka katika mataifa mbali mbali kuungana ili kufanikisha uhalifu huu. Huku wanausalama mitandao wakiangaza tu wahalifu mtandao wanaopatikana katika nchi moja moja pekee.

Bwana kamau Alitolea ufafanuzi na kusema uhalifu mtandao umekua ukiathiri zaidi makampuni ya biashara huku wahalifu wakipatikana kutoka maeneo (Makampuni) husika ya biashara. Hii inatufundisha kua Jukumu la Kujilinda dhidi ya uhalifu mtandao lazima lianzie katika ngazi binafsi.

Hivyo – Mtu mmoja mmoja na Kampuni zinapaswa kujipanga na kujiweka tayari dhidi ya uhalifu huu mtandao ikiwa ni pamoja na kuhakiki mikakati madhubuti imewekwa tayari kwa kujilinda na kubaini kwa haraka pale uhalifu mtandao unapojitokeza. Hili linaweza kufanikishwa kwa makampuni na watu binafsi kujenga tamaduni ya kujitazama mara kwa mara ili kuweza kujua hali halisi ya usalama kimtandao.

Tanzania Imepiga hatua sasa kwa kuazisha muswada utakao weza kufanikisha udhibiti wa uhalifu mtandao kuingia katika sura mpya – Hii ni kutokana na muswada wa sharia mtandao uliyoweza kujadiliwa bungeni hivi karibuni. Hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha yanayoambatana na muswada huo ili kuweza kufanya kazi yake ipasavyo yanaangaziwa. Mambo hayo yanaweza kupatikana katika andiko linaloweza kusomeka " KWA KUBOFYA HAPA" 


Aidha Kumekua na mijadala kadhaa ambayo inaweza kutoa hofu kwa wale wanao hofia muswada huo – Moja ya mijadala inaweza kusikika katika Video inayo patikana hapa.

No comments:

Post a Comment