WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Wednesday 1 April 2015

UCHAMBUZI WA SHERIA ZA MAKOSA MTANDAO, 2015

Awali ya yote nirudie kutoa pongezi kwa serikali kwa hatua hii muhimu waliyofikia ya kuwasilisha mswada wa sheria mtandao ambao naimani kubwa itakua na majibu mazuri ya kudhibiti na kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao nchini. Naomba itambulike Tanznaia si ya kwanza kuwa na sheria za usalama mitandao na ukweli ni kwamba tumechelewa kwa kiasi Fulani. Nchi nyingi tayari zinasheria za usalama mitandao na zimeendelea kuboreshwa kadri teknolojia inavyo endelea kukua na kubadilika.

Nitaanza na mifano michache kunasheria mitandao zilizopendekeza kifungo cha maisha kwa wahalifu mtandao nchini Uingereza. Na katika Kikao cha usalama mitandao kilichopita mshiriki aliyekua nami meza kuu katika kuongoza moja ya kikao aliyetokea “US Secret service” alipata kuainisha adhabu ya miaka kumi na sita bado imeonekana ni ndogo na inashauriwa kuongezwa makali.

Aidha, Nieleze ushauri wa kuhakiki sheria mitandao zinaboreshwa na kuwa kali zaidi ni kutokana na athari ya uhalifu mtandao kua kubwa sana na imekua ikimgusa kila mmoja wetu – Kwan nje ya nchi kila siku tumekua tukipata habari mpya ya matukio ya kiuhalifu mtandao ambapo maelfu wamekua wakipoteza maisha, fedha na pia ufaragha wao umekua ukitumiwa vibaya na wahalifu mtandao.

Tanzania pia hatuko salama – Nimekua nikipata malalamiko mengi ya watu kudukuliwa faragha zao, kuibiwa fedha nyingi sana na wengine kufikia hata kujitoa maisha kwa kudalilisha mitandaoni.

Hayo yote yamekua yakisukuma wataalam usalama mitandao kuumiza vichwa kuhakiki wanakuja na mwarubaini wa uhalifu huu mtandao unaozidi kuota mbawa kila kukicha. Hapo ndipo mengi yakawekwa sawa katika kukabiliana na hali hii ikiwa ni pamoja na kukuza uelewa kwa watumiaji mtandao (Matumizi salama ya mitandao), Kuzalisha na kuongezea uwezo kwa wataalam wa usalama mitandao, kuwa na sharia stahiki za uhalifu mitandao, kukuza ushirikiano kutokana na uhalifu huu kutokua na mipaka, kuhimiza kupatikana kwa takwimu sahihi za uhalifu mitandao ili kuweza kutambua maeneo athirika zaidi.

Kwenye hili la Sheria ni hatua nzuri sana ambapo Tanzania imefikia ili kuweza kurahisisha mapambano dhidi ya uhalifu mtandao nchini na kuhakiki taifa linabaki salama kimtandao. Naimani Kila mmoja wetu ukizingatia wote ni wahanga kwa namna moja au nyingine ya uhalifu mtandao lazima tufurahie na kulipokea hili kwa mikono miwili. Wataalam wa usalama mitandao wamefurahishwa sana na hatua hii yetu na pongezi ni nyingi sana hadi sasa.


Kuondoa hofu Watanzania naomba nieleze kwamba katika kuandaa muswada huu wataalam na wadau mbali mbali walishirikishwa na badae kuvuka mipaka kwa wataalam kutoka mataifa mbali mbali katika maswala haya ya usalama mitandao kutoa maoni yao na kuboresha – Haikukomea hapo imepitia hatua kadhaa na hata kupelekea kauli yangu niliyo itoa katika moja ya vikao vya wataalam wa usalama mitandao kueleza kuwa “ Hatua za kitaalam zimekwisha sasa ipo kwenye hatua za kisiasa kuweza kupatiwa Baraka kabla ya kuwasilishwa bungeni” – Kauli ambayo wataalam
waliona taifa letu linachelewa sana kwani sharia zilikua hazina shaka na hata kupitiwa kwakwe kulipaswa kua kwa muda mfupi.

Nimepata kufatilia kwa karibu kinachozungumzwa na wengi, Hofu kubwa nilizo ziona ambazo nimeona nizitole ufafanuzi ni kama ifuatavyo: -


MOJA, hofu kuwa uchunguzi wa makosa haya inaweza ikawa inakiuka faragha. Naomba nieleze kuna anaefahamu faragha yake iko dhaifu kiasi gani mara tu anavyo kua mtandaoni? Ni wazi kabisa unapaswa kujua faragha haiingi matatani tu kwa sababu ya sharia hizi mtandao.

Uchunguzi wowote wa uhalifu mitandao duniani kote unahusisha uangalizi wa kina hatua kwa hatua kwa kila ushaidi wa kielektroniki ikiwa ni pamoja na kupitia kwa karibu kila chembe ya shaka ya kile kinachoweza kuonekana kinaweza kuwa na chembe ya sababu ya uhalifu mtandao.

Uchunguzi wa makosa ya digitali ni fani na ina maadili yake – Maadili ambayo yanasomewa darasani. Maadili hayo yana hakiki mchunguzi anafata masharti na vigezo stahiki vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kutotoa siri zisizoendana na uhalifu mtandao unaochunguzwa pamoja na kuwasilisha ushahidi kwa mhusika pekee bila kushirikisha kila mtu. Zaidi inawatu maalum si kila mtu anatakiwa kushiriki katika uchunguzi wa uhalifu mtandao. Na hili kuna moja ya masharti yana sisitiza kushirikisha idadi ndogo sana ya wachunguzi ni vyema zaidi.


MBILI, kuna hofu kwanini makosa mtandao yanapatiwa ruhusa ya kuchunguzwa bila hata kusubiri ruhusa ya mahakama? Ikumbukwe kuwa kwanza uhalifu mtandao unafanyika kwa haraka sana na hauna mipaka. Ndio maana hili limeangaliwa sana na kuamua kutoa ruhusa kwa wapelelezi teule wa makosa ya uhalifu mtandao kupewa fursa ya kuazisha uchunguzi mara moja bila ya kungoja mahakama, Ikumbukwe kuna kinachoitwa “search warrant” ambacho mchunguzi wa makosa mtandao anakua nacho nahii inatolewa na kiongozi katika kitengo kinacho jihusisha na usalama mitandao katika taifa husika. Kusisitiza hili kama pangetolewa ruhusa kusubiri protokali za mahakama kufatwa kumbuka uhalifu mtandao unauwezekano mkubwa sana wa kupotezwa ushaidi wake na kusababisha ugumu kwenye kufikia malengo.

TATU, Hofu ya faragha ya kupekuliwa mawasiliano – Niulize kama unatumia mtandao kuwasiliana vizuri hofu inatoka wapi kwenye hili. Kama unajua hunachembe ya uhalifu mtandao katika mawasiliano yako sidahani kuna haja ya kua na hofu kuchunguzwa. Na ikumbukwe yule aliyetiliwa mashaka pekee ndie anaye pekuliwa si kila mmoja atapekuliwa mawasiliano yake. Hii iko kila mahali duniani sisi sio wa kwanza.

Mimi nadhani hofu kubwa tulitakiwa kuwa nayo ni kuhusu mamilioni ya pesa yanayo potea katika mabenki yetu, athari za lugha za uchochezi kwenye mitandao, athari za kuporomoka kwa maadili yetu, athari za mama na dada zetu kusambazwa picha zao za uchi mitandaoni, athari za wasanii wetu kutopata mapato kutokana na watu kuiba kazi zao mitandaoni, athari za kudukuliwa na wahalifu mitandao na taarifa zetu kutumiwa vibaya, athari za kuogopa kufanya miamala ya kifedha kupitia simu zetu, athari za kuogopa kuweka pesa benki inayo pelekea uchumi wa taifa kuyumba, athari zilizombele yetu zinazoweza kupelekea kuhatarisha maisha ( Kufa) kupitia uhalifu mtandao na athari nyingine nyingi.

Ikumbukwe athari ni kubwa sana za uhalifu mtandao na hofu kubwa tulipaswa tuwe nayo na kwapamoja tuungane kuhakikisha sharia mtandao zinazidishwa makali na uchunguzi wake unafanywa kwa kina na utaalam wa hali ya juu. Hili ndilo linapelekea wataalam tunakutana mara kwa mara kuongezeana uwezo wa kuhakiki tuna tambua mbinu mpya za uhali mtandao na kujinoa kujua namna ya kuchunguza na kuweza kufikia malengo ya kudhibiti.

Wabunge walionyesha hisia zao kutaka kupata ufumbuzi wa mabilioni ya pesa yanayopotea katika mabenki na makampuni ya simu kupitia uhalifu mtandao – Wanapaswa kukumbuka udhibiti unapaswa kwenda sambamba na kua na sheria madhubuti zinazoweza kuhimili hali mbaya ya uhalifu mtandao nchini.


Naomba tu kusisitiza watanznaia kusoma na kuelewa na sio tu kufata mikumbo kwenye hili. Aidha, Hofu kubwa lazima iondoshe hofu ndogo. Nikiimanisha Uhalifu mtandao nitishio kubwa kuliko ugaidi na sheria zetu zanafanana kabisa na sheria nyingine za mataifa mbali mbali huku baadhi zikiwa kali zaidi kuliko tulizo nazo. Nimalizie kwa kutoa wito wa matumizi salama ya mitandao ili kujiepusha na kuingia matatani bila sababu za msingi. Huku nikiwatoa watanznaia hofu juu ya uchunguzi wa dhati wa makosa haya uanafanywa na hakuana atakae ingia matatani kama si muhusika.

13 comments:

  1. Kileo umenifurahisha sana na maelezo yako mazuri, Uwezo wako wa kuelezea umedhihirisha kua ni mkubwa sana mtaalam wetu! Your brother Johson Kimeri Nipo Shinyanga.

    ReplyDelete
  2. Hellow Kileo, ni dhairi kwamba ungeupitia huu mswada nadhani ungegundua una mapungufu mengi sana. Moja ni mambo mengi hayana tafsiri halisia ya kinachotegemewa kifanyike na mswada huu. Pili kuna vitu vimechukuliwa kwenye sheria za nchi nyingine ambazo hazitaweza kutekelezeka katika mazingira yetu. Tatu huu mswada ulitakiwa utafsiriwe na wataalam wa mambo haya kwa wana sheria ili ukae kwenye lugha ya kisheria na uweze kufanya kile kinachotegemewa au tarajiwa. Na mwisho ningependa kushauri tu kuwa na sheria bila kuwa na uwezo wa watu wenye uwezo wa kitaalamu wa kuyaweka yale yanayosemwa kuwa ni makosa ya kimitandao kuonekana makosa haitatusaidia kufikia malengo tunayoyatarajia huu mswada kuyafanya. Nchi kubwa duniani zilizoendelea wana hizi sharia na mafanikiao yake yamewezeshwa na uwezo wa kitaalamu wa kupembua na kuyabaini makosa hayo na si kwa kuwa na sheria tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwanza kabisa nashkuru kwa maoni yako - Labda naomba nikujulishe tu kua mimi binafsi Fani yangu halisi ni usalama mitandao na uchunguzi wa makosa ya kidigitali ambapo nimesomea katika ngazi ya degree na baadae kuongeza ujuzi katika ngazi ya Masters. Nimetangulia kulisema hili kutokana na sababu kwamba sheria mitandao ni moja ya vitu nimevipitia na moja ya mitaala niliyo itumia nimesha ileta nchini ili kuweza kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kuwaongezea uwezo wataalam wetu.
      Kama umekua ukifatilia kwa karibu nimekua niki himiza sana sheria kuambatana na uelewa kwa wananchi juu ya sheria hizo pamoja na kuwaongezea uwezo watu wetu wanaoshughulikia makosa haya kuweza kwanza kabisa kuzitafsiri sheria hizi na kujua namna ya kuzifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo stahiki wa kuziendea kitaalam maana hii ni fani na ina taratibu zake.
      Lakini pia nimeanisha kwa kina sana kuwa - Siku zote Hofu kubwa inatakiwa iondoe Hofu ndogo ( Uhalifu mtandao una athari kubwa sana kwa taifa na dunia kwa ujumla hasa hapo baadae) hivyo kuwepo na sheria hizi zitasaidia kuweza kudhibiti na kutoa fursa ya kuhimili vishindo vya uhalifu huu.
      Aidha, Nisistize tu kua Uhalifu mtandao Duniani kote unafanana na ndio maana unaitwa BORDER LESS CRIME - UHALIFU USIO NA MIPAKA. hivyo sheria kufanana na nchi nyingine sioni tatizo.
      Mwisho kwa swala la kupitia - Nimepitia na mapungufu ya kibinaadam ya kawaida ya kimaandishi ( Mfano Kutaja Kiwango cha chini bila kutaja kiwango cha juu cha mtu kuwekwa ndani) hayawezi kunifanya nione haufai . . . Na hii ndio maana tunasema Sheria mitandao zinapitiwa mara kwa mara na kuboreshwa kutokana na ukuaji wa teknolojia una ambatana na mabadiliko ya teknolojia inayopelekea mbinu mpya za uhalifu mtandao kufanyika ( Sheria zilizo wasilishwa sasa sio fixed through out life time).

      Kama kuna maeneo unadhani ni ya kuweka sawa ya kimaandishi - Hili litafanyiwa kazi kwenye review.

      Ahsante sana.

      Delete
    2. Jabhera Matogoro2 April 2015 at 21:25

      Binafsi maelezo uliyoyatoa Kileo Ni mazuri na kuwatoa wadau hofu juu ya wataalamu. Naomba kwanza ku-declare interest kuwa Mimi Ni Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dodoma katika College of Informatics and Virtual Education. Baada ya kuona changamoto zinazoikabili nchi juu ya wataalamu WA kulinda mitandao yetu tulianzisha degree ya BSc. In Computer and Information Security toka mwaka 2008/2009 na mpaka sasa tunao vijana WA kitanzania wengi ambao wamemaliza katika fani hiyo na kwa kiasi Fulani wanaendelea kusaidia nchi katika idara mbali mbali ikiwemo usalama WA taifa, jeshi, polisi n.k na kwasasa tupo kwenye mchakato kutoa Masters in Information Security and Assurance ambayo PIA inachukua vijana wengi wengi WA kitanzania na hivyo kusaidia kujenga vijana wetu wenye ujuzi WA kutosha.

      Mwisho, sheria hii naona imechelewa Kuja na sisi kama wataalam tunaiona hii Ni hatua kubwa. ILA wazi lililotolewa na mdau juu ya kushirikisha watu WA sheria na nadhani lilikuwa zuri na naamini wameshirikishwa ili kutoa tafasiri za kisheria hasa utekelezaji ukianza.

      Delete
  3. Mimi nadhani hapa Tanzania ilipofika ndipo hasa pa kuanzia,kama mtaalamu anavyosema ni muhimu kuangalia kuweka sheria lelemama ili watu waogope kutumia teknolojia kwa vile kuna watu wanaotaka kuendelea kuiba na kutukana watu na kuweka picha za ngono?au kuweka sheria ngumu ila kila anayetumia mtandao kuwa na uoga wa kufanya uhalifu kupitia mtandao.
    La pili ni serikali iwaambie wananchi kuwa ina wataalamu wangapi na kama wapo vifaa vipo ?au ni ujanja wa kuwapa watu kesi za mtandao na kuchukua muda kufanyiwa uchunguzi?Je majaji nao wanajua kuhusu hizi kesi?je wanasheria wanajua?
    Ni nini unachofanya sasa hivi kama mtaalamu kuhakikisha wananchi wanaepuka kufanya makosa kwa kutokussudia?

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwanza nashkuru kwa maoni yako.
      Natambua kuna Uhalifu mtandao unafanyika pasi na kusudia.
      Nimesha andikia mara kadhaa kuhusiana na concern yangu ya AWARENESS PROGRAM pamoja na maboresho yake kwani iliyopo sasa inahitaji Improvement kiasi na msisitizo zaidi.
      Aidha, mimi Binafsi nilisha endesha mafunzo kwa wachunguzi wetu wa makosa mtandao nchini kuhakiki kunapatikana uwezo mzuri wa kukabiliana na uhalifu huu - Point hapa ya msingi ni kwamba natambua kuna mahitaji ya Capacity building kwenye hili ( Hasa ukizingatia ni Kitu kipya bado kwa wengi)

      Nashkuru sana kwa mchango wako.

      Delete
  4. Brother Kileo,
    Shukran kwa ufafanuzi mzuri na natumai kwa watu watakao pitia jinsi ulivyofanya uchambuzi huu nadhani wataelewa na kuona manufaa ya Sheria hii kwa wakati huu na ujao, kwani kasi na ukuaji wa watumiaji wa mtandao unazidi kukua kwa kasi sana. Hivyo natumaini sheria hii inasaidi kwendana na kasi hiyo ili isilete madhara ambayo tunaweza kuyaepuka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nashkuru sana Salum Kwa maoni yako.

      Ahsante.

      Delete
  5. Wewe unaishi Tanzania?Haya yote unayosema ni kwenye vitabu lakini mahakama na vyombo vyote vilivyopaswa kuwa vya haki nchini havifuati hivyo ukiwa na pesa ndio utanunua haki.!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi Ni Mtanzania na Baada Yakupata Elimu yangu Nje - Nimesha rudi Tanzania Mkuu.

      Hili la Kununua haki, Ni mapungufu yapo kila mahali na si tu kwamba litakuwepo kwenye sheria hizi mtandao pekee.

      Ahsante sana kwa Mchango wako.

      Delete
    2. Asante sana Ndg Kileo.
      Mimi ningeshauri pamoja na sheria elimu itolewe kuhusu hatari za mitandaoni, kwani mtandao unaunganisha dunia kuwa kama kijiji.Kwa mfano wengine wanatoa program za bure kama 'antvirus' je tutajuaje kama hizo programs ni salama au la. Kwani Watanzania wengi hatuna ufahamu wa kutosha juu ya hizi progams.

      Delete
    3. nasjkuru kwa maoni yako.
      Nachoweza kusema tu ni kua kubwa ambalo limekua tukilipigia kelele sana katika vikao vyote vya kiusalama mitandao maeneo yote hili la Awareness ni namba moja na pia kuna mengine mengi tu ya kufanyiwa kazi ili kufikia malengo.

      Ahsante.

      Delete