Naimani Mwaka huu Tanzania ita uchukulia mwezi huu kinamna ya kipekee ili kuweza kukuza uelewa kwa watu wake Tukio ambalo nategemea makampuni mbali mbali na maeneo mengine yataandaa program mbali mbali za kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao ili kuweza kufikiwa malengo yaliyokusudiwa na wanausalama wote mitandao duniani kote.
Aidha, inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo la uhalifu mtandao. Tatizo kubwa kubwa ni kua njia hizi zimekua zikiishia katika maandishi baada ya kujadiliwa na wanausalama mitandao ambapo mimi binafsi nilikua miongoni mwao.
Leo
nitaangazia njia ambayo imeshika nafasi ya juu na imeonekana na uwezo mkubwa wa
kuhimili uhalifu mtandao ambapo imeaminika inauwezo wa kupunguza aina mbili za
wahalifu mtandao pamoja na kusababisha aina ya tatu kupungua makali. Kwa ujumla
wake imezungumzwa inaweza kupunguza hadi asilimia 71% ya uhalifu wote mtandao
kama itafatwa vizuri na kupewa uzito wa kipekee katika mataifa yote.
Njia
hii si nyingine bali ni “Awareness
Program” Yaani elimu ya uelewa wa uhalufu mtandao na namna ya kujilinda.
Elimu hii inatoa fursa kwa mwananchi wa kawaida kutambua aina mbali mbali za
uhalifu mtandao, athari zake, njia ya kujilinda, Na Namna ya kulinda wenzake.
Kwa
kupata elimu hii wale wote waliokua wakifanya uhalifu mtandao pasi na kujua
wanakua na ufahamu wa kutosha na hatimae kundi hili linakua limeondokana na
uhalifu mtandao. Aidha, kundi la pili ambalo ni lile linalofanya uhalifuu huu wa mtandao wakiwa hawana namna kwa kutokujua athari zake baada ya kujua athari za uhalifu mtandao kwao
na kwa wengine na pia kujua njia mbadala wanazoweza kutumia kuepukana na
uhalifu huu kupitia elimu ya uelewa ya usalama mitandao kundi hili linaweza pia likapunguzwa hadi asilimia 84% kwa mujibu wa wataalam
wa usalama mitandao.