Mwezi
Huu wa October, Nimekua na kazi kubwa ya kuhimiza mashirika, makampuni pamoja
na Taifa kwa ujumla kuutumia vizuri kutokana na kua ni mwezi maalum uliotengwa
na wanausalama mtandao kote duniani wa kukuza uelewa wa matumizi salama ya
mitandao ili kuweza kupunguza wimbi kubwa la uhalifu mtandao duniani kote.
Nategemea
kuandikia yaliyo jiri Nchini kwetu hapo baadae ili kuweza kujua namna mwezi huu
tulifanikiwa kukuza uelewa kupitia mashirika mbali mbali na taifa kwa ujumla
wake. Kitu ambacho niliweza kukiwasilisha ndani ya mwezi huu ni Maazimio ya
namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao katika ngazi ya Taifa, Bara Na Duniani
kwa ujumla ambapo ni maazimio tuliyo kubaliana kimsingi tulipo kutana Mwaka
huu mwezi wa Tano Nchini Afrika kusini.
Wakati
nikiwasilisha mada hiyo nimeweza kuulizwa swali la ni jinsi gani maazimio hayo
yanaweza kuambatanishwa kwenye ngazi ya Kampuni ndogo ndogo na mashirika mbali
mbali ili ambacho nimekua nikihubiri yakua lazima swala la ulinzi mtandao
lianzie kwenye ngazi ya mtu binafsi, Makampuni na kuendelea hadi kufikia Dunia
nzima kuweza kufanyiwa kazi na kuonyesha Impact.
Nimeamua
kuandika andiko hili maalum ambapo nitafafanua Njia Kuu kumi (10) ambazo makampuni na mashirika wanaweza kutumia
kukabiliana na uhalifu mtandao sanjari na kuonyesha yanavyo wiana na maazimio
tuliyokubaliana kimsingi ambapo yatasaidia kukabiliana na uhalifu mtandao
katika ngazi ya kitaifa hadi kidunia.
Mambo
yenyewe ni kama ifatavyo:-
MOSI,
Toa elimu ya uelewa ya uhalifu mtandao kwa wafanyakazi – Asilimia zaidi ya 50%
ya udukuzi ulifanikiwa kutokana na mapungufu yaliyo fanya na binaadamu ambapo
kutokana na uelewa mdogo wahalifu mtandao walifanikisha kuingilia/ kudukua
makampuni mbali mbali na kusababisha hasara kubwa. Hii inaendana na Azimio la
“Awareness programs” ambapo ndio limeendelea kufanyiwa kazi na ndio
limesababisha “Cybersecurity awareness month” kusisisitizwa sana.
PILI,
Waongezee uwezo wafanyakazi wako – Kumekua na uhaba wa wajuzi wanaojua maswala
ya usalama mitandao sanjari na wanaojua kushindwa kujiendeleza mara kwa mara
hasa ukizingatia ukuaji wa teknolojia unaambatana na ukuaji wa mbinu mpya za
uhalifu mtandao. Hivyo kuongezea uwezo wafanyakazi wako mara kwa mara
utawafanya waweze kufahamu vitu vipya vitakavyo wawezesha kukabiliana na mbinu
mpya za wahalifu. Hili linaendana na azimio la “Capaciti Builing” ambapo
tuliazimia kuhakiki tunakuza na kuongeze uwezo wataalam wa usalama mitandao
duniani kote.
TATU,
Wekeza katika vitendea kazi vya kuzuia uhalifu mtandao – Ni wazi kabisa lazima
kila kampuni iwe na njia madhubuti za uwekezaji katika vifaa mbali mbali
ambavyo vitafanikisha kukabiliana na uhalifu mtandao kwenye kapuni. Hili
litaendana sambamba na azimio lililopewa jina la “Tools” ambapo tuliangazia
sababu za vitendea kazi vya kusababisha uhalifu mtandao kupatikana kwa gharama
ya chini au bure kabisa wakati upande wa vinavyo zuia vimekua vikipatikana kwa
gharama za juu sana na kuazimia wanaohusika kutafuta njia rafiki ya kuweza
kusababisha upungufu wa bei wa vitendea kazi ya kukabiliana na uhalifu mtandao
ili kuweza kufikia malengo.
NNE,
Hakikisha usalama mtandao wa Kampuni unaangaziwa na wajuzi – Kumekua na wimbi
kubwa la uhalifu unaoshindwa kugundulika kwa wakati kutokana na waangalizi
kutokua na ujuzi wa kutosha wa kubaini, na kuchukua hatua pale wahalifu mtandao
wananpo leta maafa kwenye makampuni. Hii inasababisha hata makabiliano na
uhalifu mtandao katika ngazi ya kitaifa au dunia kua ngumu kutokana na kua na
wimbi kubwa la makampuni kutokua na watendaji sahihi katika maswala ya usalama
mitandao ambayo yanaendelea kuathiri mataifa. Hii inaendana sambamba na Azimio
la “Right skill set” ambapo tulikubaliana kimsingi lazima changamoto ya kuwa na
wapambanaji na uhalifu mtandao kua na ujuzi mdogo na kutegemea kupambana na wahalifu
wenye ujuzi mkubwa lazima iangaziwe na lazima tuwe na wajuzi sahihi
watakaowezesha kufikiwa kwa malengo katika mapambano na uhalifu mtandao.
TANO,
Jenga tabia ya ukaguzi wa usalama wa mitandao ya kampuni – Pamekua na tabia ya
Kampuni kuwekeza kwenye TEHAMA iliyo ambatanishwa kwenye mitandao na kusahau
kuifanyia ukaguzi wa mapungufu iliyonayo yanayoweza kuwarahisishia wahalifu
kuingilia kampuni. Njia hii kitaalam inajulikana “vulnerability assessment” au
“Penetration Testing” ambapo utaweza kujua mapungufu mifumo yako inayo na namna
ya kuziba mapungufu hayo. Makampuni au mashirika mbali mbali yamekua
yakihamasishwa kua na tabia ya kufanya ukaguzi huu walau mara moja kwa mwaka
ili kuweza kuziba mianya yoyote inayoweza kupelekea wahalifu kupenya na kufanikisha
udukuzi katika kapuni.
SITA,
Unapoingiliwa na wahalifu mtandao toa taarifa mapema – Makampuni yamekua
yakiugulia uharibifu mkubwa unaofanywa na wahalifu mtandao na kuwasababishia
wahalifu hao kuendelea kufanya hivyo wakijua hakuna kinacho ripotiwa. Hii si
sawa lazima kila kampuni inapopata maafa ya uhalifu mtandao itoe taarifa mara
moja kwenye maeneo husika ambapo njia stahiki za kukabiliana na uhalifu
uliokukumba ili kuweza kuwawajibish wahusika na kutengeneza takwimu sahihi
ambazo zitawezesha kujua aina za uhalifu zinazo shika kasi ili kuweza
kuzitaftia suluhu ya kudumu ili isijirudie iweze kupatikana maramoja. Hii
linaendana na azimio la “Statistics” Ambazo tulikubaliana tunapo kua na takwimu
sahihi zitapelekea kuweza kujua uhalifu unao kua zaidi na kupatia suluhu ya
haraka nay a pamoja kuweza kukabiliana nao.
SABA,
Angazia macho kila kinachoingia kwenye mtandao wa kampuni – Hii ni maarufu sana
kwa jina la “Monitoring web traffics” ambapo kila kinachoingia na kutoka
kinaangaziwa kwa karibu na inapo bainika kuna kinachotatanisha kuingia kwenye
mtandao wako unachukua hatua za haraka kukizuia ili kuendelea kubaki salama.
Pamekua na mafanikio makubwa kwa kampuni zilizojijengea kuangazia macho hili
ambapo wahalifu wanapo jaribu kuingia wamekua wakigundulika mapema.
NANE,
Hakikisha kila aina mpya ya uhalifu mtandao unaifahamu – Wengi wameendelea kua
waathirika na uhalifu huu mtandao kutokana na kutokua na tabia ya ufatiliaji wa
aina mpya ya uhalifu mtandao pamoja njia mpya ili kuweza kujipanga mapema na
namna ya kukabiliana nazo kabla hazija kufikia. Hapa nitolee mfano wa “Click
Jacking” Ambapo Iliweza kuathiri wengi kutokana na wengi hawakujua aina hii ya
mbinu ambayo wahalifu mtandao walitumia kufanikisha malengo mbali mbali ya
kuleta maafa kwenye mitandao yetu.
TISA,
Kua Makini na Mitandao ya kijamii – Kumekua na changamoto kwenye makampuni mengi
kutokana na kuweka taarifa zao nyingi kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na
kazi zinazoendelea na kusahau taarifa hizo ambazo zinaweza kuonwa na yeyote
zinaweza kutumiwa vibaya na wahalifu mtandao ili kufanikisha moja ya njia za
ukusanyaji wa taarifa kutoka kwenye kampuni lengwa ya kufanyiwa uhalifu ili
kuweza kufikia malengo. Njia ambapyo ni maarufu kama “Reconnaissance”.
KUMI,
Kujenga tabia ya kujiwekea kopi ya taarifa zako zilizoko mtandaoni – Kibaya
kuliko vyote ni pale kampuni inaingiliwa/dukuliwa na wahalifu mtandao
wanafanikiwa kuiba taarifa za ampuni huku hukua umejpanga kua na taarifa hizo
mahali pengine. Kitaalam tunaita “Backup” ambapo mara nyingi zinakua katika
mtandao tofauti ambapo taarifa zinapo potea basi kampuni haingii katika hasara
kwani itaelekea kwenye kinachofahamika kama “Offsite back-ups” au “mirrored
servers” kuweza kupata kile kilicho ibiwa na kupotezwa.
MENGINE,
Zaidi ya hayo kumi niliyo ainisha kulikua na maazimio mengine ambayo yanaweza
kutumika kama nyongeza ambapo yanaweza kuongeza msaada hasa kwenye ngazi ya
kitaifa ingawa Makampuni pia yanaweza kuangalia namna wanaweza kuyafanyia kazi.
Mambo
hayo ni pamoja na Ushirikiano baina ya kampuni na kamuni, Hili ni kushirikiana
kwenye taarifa za viashiria vya uhalifu mtandao, Nyingine ni kuondoa
ukiriritimba wa kua na mlolongo mrefu wa kukabiliana na hali ya hatari ya
uhalifu mtandao, Kuwa na Kanuni, Sheria ambazo zitawezesha kuweka mambosawa na
mwisho kuhakiki panakua na kufanyiwa kazi yote yaliyo jadiliwa na sit u kuishia
kwenye mazungumzo au maandishi.
Mambo
haya yanaingia kwenye maazimio ya – “Collaborations – Cyberlaw (Legal
framework) – bureaucracy and Time for Action.” Ambapo kwa ujumla wake
tulikubaliana kimsingi hakuna namna ila kuhakiki tunatambua ili kufikia malengo
lazima yote yawe katika ubora stahiki ili kuweza kufanikisha vita dhidi ya
uhalifu mtandao duniani kote.
Umenena vizuri sana kaka
ReplyDeleteNakukubali vibaya mno.
Mdogo wako Salmin.
0713452429
Nashkuru sana - Nakutakia kila la kheri.
DeleteKiongozi, umeweka bayana kila kitu. Mda wa kufanya vitendo sasa, hususani juu ya 'Capacity Building' . Tupo pamoja kiongozi katika hili suala.
DeleteNashkuru sana kaka - Indeed Knowledge ndio tools kubwa kupambana na Uhalifu Mtandao.
DeleteKila la Keri Brother Shiliba.