WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Tuesday 13 October 2015

MKUTANO WA WAKUU WA TEHAMA WAMALIZIKA NCHINI KENYA

Kwa mara nyingine CSK kwa kushirikiana na wadau wengine wamefanikiwa kuandaa mkutano ulio husisha wakuu wa TEHAMA ambapo mambo mbali mbali yalipata kujadiliwa. Katika mkutano huo ambapo Binafsi nilikua  Mwalikwa Rasmi ambapo pamoja na mambo mengine niliweza kutoa mafunzo ya namna ya kufanikisha upelelezi wa kitaalam wa uhalifu mtandao pamoja na hali halisi ya uhalifu mtandao duniani kote.

Aidha, Nilipata pia kuzindua kampeni ya Mwezi wa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao na kuweza kutoa wito kwa wakuu hao kudumisha utamaduni huu mzuri unaoweza kutoa msaada mkubwa kukabiliana na uhalifu mtandao duniani kote.

                      

Pia katika hatua nyingine nilipata kubadilishana mawazo na aliyekua Raisi wa naijeria Generali Obasanjo, ambapo pamoja na mazungumzo mengine nilionesha ndoto yangu ya kuona wakuu wa Nchi za Afrika kuzungumzia swala hili la uhalifu mtandao kwani athari zake zinaonekana wazi na zimekua zikisababisha kuzorotesha Uchumi, Utamaduni, Siasa, Jamii na kadhalika.


Mataifa Ya Ulaya , Asia, Mashariki ya kati na Marekani kupitia wakuu wao wa Nchi tumeshuhudia wakijadili kwa mapana athari kubwa zinazotokana na uhalifu mtandao ambapo jitihada za dhati zimeendelea kuonyeshwa ili kukabiliana na hali hiyo.



Tukiendelea na Vikao Nchini Kenya Benki ya I & M ya nchini humu ilitangaza kusitisha huduma zake za kimtandao kutokana na kukithiri kwa uhalifu mtandao ambapo pesa nyingi zimekua ziki potelea humo.

Itakumbukwa ni hatua kadha wa kadha zimechukuliwa baada ya wizi katika ATM kukithiri ambapo ulinzi zaidi wa kiteknolojia ulielekezwa huko na kusababisha hali hiyo kupungua kasi. Wahalifu mtandao pasi na kurudi nyuma wakabuni njia mbadala na kufanikiwa kuhamishia uhalifu huo katika miamala inayofanywa kupitia mitandao.



Wahalifu hawa wa mitandao wakasababisha hali kua tata zaidi kwa mabenki kadhaa duniani Huku Bank ya I&M kuwa ni miongni mwa wa athirika na hatimae kusitisha huduma zake. Hali hii inatufunza wa Tanzania kujua Wengine wamenyolewa na Sisi Lazima tutie nywele maji.

Bado Uhalifu mtandao Unakua na jitihada zilizopo ni lazima pia ziweze kuendana sambamba na kujua kila mmoja wetu anadhamana ya kutumia mitandao katika hali salama. Kwa kufanya hivi kutakua na mafanikio ya kupunguza uhalifu huu kwa kiasi Fulani.

    

Aidha, Nisisitize tena Tupo katika mwezi wa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao ambapo dunini kote wana azimisha kwa shughuli mbali mbali sahihi za kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao “Cybersecurty awareness Month” ambapo ni miongoni mwa njia za juu na madhubuti zinaz aminika zinaweza kusaidia kuhimili vishindo nya uhalifu mtandao.

Katika hutuba zangu wakati wa mkutano huo wa wakuu wa TEHAMA, Siku sita kuendelea kuhimiza ushirikiano baina ya watu binafsi, Makundi ya wataalam, makampuni, Nchi pamoja na mabara ili kuweza kufikia malengo ya kukabiliana na kukithiri kwa uhalifu huu mtandao huku nikitolea mfano ushirikiano mkubwa ulioko baona ya wahalifu ambapo marazote wamekua wakifikia malengo.



Ukweli utabaki kua ya kua hakuna Taifa lolote linaloweza kukabiliana na uhalifu mtandao likiwa limejitenga. Tunamsemo maarufu tunaosema “No one can fight cybercrimes in isolation” – Hivyo hakuna budi kuliangazia hili ili kuweza kufikia malengo.

Kwa upande wa maendeleo ya Mwezi wa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao, Tanzania kumeendelea na matuio kadhaa kupitia kampuni ambapo mafunzo yamekua yakiendelea. Pia Kwa mwaka huu nafurahi kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari kwenye hili kwani mchango wao umeonekana kua wa manufaa makubwa kabisa.

Natambua Kituo cha redio cha Morning Star Kwa kuona umuhimu wa mwezi huu na kutenga Dakika 10 kabla ya saa mbili usiku kila siku kushiriki katika kutoa elimu ya matumizi bora ya mitandao ambapo matukio yanayofanyika pia yanaweza kutumia muda huo kushirikisha wengine kwa kile kinacho fanyika katika mwezi huu maalum.

No comments:

Post a Comment