Uhalifu
mtandao bado umeendelea kukua maeneo mbali mbali Duniani – Tishio hili
linachukua sura ya kipekee wakati ambapo uhalifu mtandao ume endelea kufanyika
kwa ustadi wa hali ya juu huku ukindelea kukua kwa kasi ya kipekee.
Ujuzi
mkubwa walionao wahalifu mtandao unatosha kua somo kwa wanaopambana na uhalifu
mtandao kujipanga zaidi hasa ukizingatia namna ya ufanyai uhalifu mtandao,
umeendelea kubadilika kadri teknolojia inavyobadilika sanjari na inavyokua.
Kuzingatia
yote haya moja ya maazimio tuliokubaliana Jijini Johannesburg, Afrika kusini
mwaka jana (2015) ni kuhakiki ya kua situ tunakua na watu sahihi wenye ujuzi wa
kupambana na uhalifu mtandao bali pia kujenga tabia ya kuwaongezea uwezo na
kutengeneza nguvu kazi zetu zitakazo saidia mapambano dhidi ya Uhalifu Mtandao
Barani na Duniani kwa ujumla.
Nchi
mbalimbali barani zimeendelea kulifanyia kazi hili ikiwa ni pamoja na kupitia
upya mitaala yake ili kuhakiki elimu sahihi ya maswala ya usalama mitandao
inafundishwa na kuhimiza tabia ya wahusika kuendelea kupatiwa mafunzo ya mara
kwa mara pamoja na kujijengea tabia ya kujifunza kwa kupitia yale yanayo andikwa
na wataalam wa usalama mtandao ili kufahamu kinachoendelea katika fani husika
kwani Mbinu za kihalifu mtandao zimekua zikibadilika sana kadri teknolojia
inavyo badilika pamoja na kukua.
Binafsi,
Nilipokea mwaliko katika Kauti ya Bungoma Nchini Kenya ili kushuhudia na
kushauri mpango mpya wa kauti hiyo wa kuanzisha maabara maalum zilizo dhamiriwa
kua ni za kutengeneza wataalam wa usalama mitandao watakao saidia kukabiliana
na uhalifu mtandao si katika kauti pekee bali ni pamoja na Nchi nzima ya Kenya.
----------------------------------------
NEWS UPDATES: A new free online tool for the
notification of personal data breaches has been developed by ENISA, in
co-operation with the Office of the Federal Commissioner for Data Protection
and Freedom of Information of Germany (German DPA).
The
purpose of the tool is to allow data controllers to complete and submit online
a personal data breach notification to the competent authority.
----------------------------------------
Nilikubali
mwaliko huo, na nilipo zuru Kauti hiyo nilipata kushiriki mambo kadhaa. Kubwa
ikiwa ni kutembeea Mradi huo wa uanzishwaji wa Maabara maalum ya kutengeneza na
kukuza vipaji katika fani ya usalama mtandao sanjari na kuzungumza na wanafunzi
wanaodhaminiwa na serikali ya Nchi ya Kenya ili kuweza kutengeneza mifumo mbali
mbali itakayoweza kutumika katika simu.
Katika
mazungumzo yangu na Vijana hao nili wahimiza kuwa natabia ya kujisomea mara kwa
mara maswla ya usalama mtandao ili kujua yanayojiri na suluhu mbali mbali zinazoendelea
kupatikana kutoka kwa wataalam wa uslama mitandao wanaopatikana maeneo yote
duniani.
Aidha,
Niliwataka wasiwe tu wanajifunza ili kuweza kujua na kuwa wataalam tu wa
maswala ya usalama mtandao bali wajue wanatakiwa kuwa na uzalendo wa dhati na
kujua wanadhamana kubwa ya kuhakiki wanakabiliana ipasavyo na uhalifu mtandao
ili baadae na wao wasijikute wametumbukia katika vitendo vya kihalifu mtandao.
---------------------------------------
NEWS UPDATES: Fast-food chain Wendy's says a
cyberattack that stole payment card details affected 1,025 U.S. restaurants
owned by franchisees, a far higher figure than first estimated.
-------------------------------------------
Shughuli
nyingine nilizo pata kushiriki ni pamoja na kushiriki mahafali ya wahitimu wa
chuo kimoja katika kauti hiyo sanjari na kuzuru Chuo kikuu cha Kibabii ambapo
pia nilipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa Shahada ya Uzamili wa maswala
ya TEHAMA.
Katika
mazungumzo yangu na wanafunzi hao niliwahamasisha kujenga tabia ya kujifunza
fani hii ya usalama mtandao kwani kwa sasa imeendelea kua muhimu sana maeneo mengi
sanjari na kuwahimiza waifunzapo maswala ya usalama mtandao wajitahidi kuwa
katika upande wa kuzuia na wasije kua ni changamoto kwa kupelekea ukuaji wa
Uhaliffu mtandao.
Nichukue
fursa hii kupongeza juhudi za serikali ya Kauti ya Bungoma ya nchi ya Kenya kwa
kuanzisha mpango huo muhimu ambao naimani kubwa utakua na Manufaa makubwa hasa
kipindi hiki ambacho wahalifu mtandao wameendelea kua na mbinu mpya madhubuti
za kutekeleza uhalifu mtandao na nimategemeo yangu zao la jitihada hizi litakua
chanya na kua msaada mkubwa kwa taifa hilo la Nchi ya Kenya katika upambanaji
na uhalifu mtandao.
Aidha,
nitoe wito kwa mataifa mengine hususan mataifa ya jumuia ya Afrika mashariki
kujua wana dhamana ya kuhakiki rasilimali za jumuia ya Afrika mashhariki zinaendelea
kulindwa ipasavyo dhidi ya wahaifu mtandao – Hivyo pawe na dhamira ya dhati za kuhakiki
tunaendelea kutengeneza watu wetu katika fani hii ambao watakua ni msaada kwetu
katika kukabiliana na uhalifu mtandao.
No comments:
Post a Comment