Mataifa
mbali mbali yame endelea kuwekeza katika sekta ya TEHAMA ikiwa ni katika
jitihada za kurahisisha upatikanaji wa mawasiliano kwa wanchi wake pamoja na
kukuza ufanisi katika utendaji kupitia utumiaji wa mifumo ya Digitali/Tehama.
Teknolojia
ya Setilaiti imeongeza chachu kwenye hili na kwa kuliangalia hili Jijini Addis
Ababa Nchini Ethiopia mkutano wa kwanza kwa nchi za Africa wenye kauli mbiu
“Digital Skies – Everyone connected”
ulipata kujadili kwa kirefu maswala mbali mbali yahusuyo TEHAMA ambapo
Viongozi mbali mbali na wataalam katika nyanja hii walipata kuwasilisha mada na
kushiriki katika mijadala mbali mbali.
Waziri
wa TEHAMA wa Nchi ya Somalia Mh. Jamal Hassan alikua ni mingoni mwa walio
zungumza, ambapo ali ainisha TEHAMA inavyo endelea kukua kwa kasi nzuri katika
taifa lake.
Mwanzo
wa kuwasilisha mada yake alianza kwa kusema, Somalia imekua na umaarufu mkubwa
katika maswala ya ugaidi, Lakini Nchi imepiga hatua nzuri katika kuwekeza katika
sekta ya TEHAMA.
Akifafanua
alieleza taifa lake (Somalia) linatumia huduma ya fedha mtandao na fedha
kupitia simu ambapo wafanyakazi wake wana endelea kulipwa kupitia simu za
mkononi. Aidha, Aliainisha mifumo mbali mbali imeendelea kuwa ya kidigitali ili
kuhakiki ufanisi unakua.
Aliongeza
kwa kusema wananchi wa taifa hilo wameendelea kua na matumizi makubwa ya
mitandao ikiwepo mitandao ya kijamii inayo rahisisha mawasiliano baina yao.
Alizungumza pia mpango wa Nchi yake kupata huduma ya Mkonge ambao alisema
utatokea Dar-es salaam hadi Nchini mwake.
Kwa
ufupi alianisha jitihada mbali mbali ambazo, pia taifa la Tanzania limeendelea
kuwekeza kwa kiasi kikubwa na tayari kama taifa tumepiga hatua kubwa sana.
Baada
ya kuwasilisha mada yake nilipata kufanya nae mazungumzo waziri huyo wa
Somalia, ambapo kwanza nilimpongeza kutokana na ukweli kwamba sikua nafahamu
mengi aliyo yazungumza na sikuwahi kudhania kutokana na mengi tunayo yasikia
kutoka kwenye taifa hilo.
Lakini
pia, Nilionyesha wasi wasi wangu kwake na kunukuu ripoti ya usalama mtandao ya
mwaka huu ambayo tayari nilisha ijadili na kumwambia ilionyesha taifa lake ni
miongoni mwa nchi zinazo athirika zaidi na mashambulizi mtandao/ Uhalifu
mtandao katika ngazi ya kidunia.
Nikamuuliza
nchi yake ina mikakati gani kukabiliana na hali hiyo – Aliita watendaji wengine
akiwemo katibu mkuu wa wizara yake na Mkuu wa kampuni ya simu ya nchi hiyo ili
kuweza kuzungumzia hili.
Nilicho
gundua katika mjadala wangu na wao ni kwamba kama ilivyo katika mataifa mengine
barani Afrika, Uwekezaji katika sekta ya TEHAMA hauendani sambamba na usalama
wake kitu ambacho kimeendelea kusumbua mataiffa mengi ya kiafrika.
Mwisho
wa mazungumzo yetu , Waliamua kunialika Nchini mwake na wali nitaka katika
matembezi yangu niweze kutazama walicho fanya na kuwashauri zaidi katiaka sekta
ya usalama mtandao. Mwaliko ambapo nili
muahidi kujitahidi kutafuta wakati na kutembelea Taifa hilo.
Mada
nyingine ni ya Gavana wa Kauti ya Bungoma, Kenya Mh. Kenneth Lusaka ambapo iliweza
kufafanua vizuri umuhimu wa mataifa kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya TEHAMA
ambapo kama walivyo zungumza watangulizi wengine ali weza kuainisha hatua kubwa ambayo Kaunti anayo iongoza imepiga katika sekta ya TEHAMA huku akitolea mfano wa
mfumo wa ukusanyaji mapato kupitia TEHAMA ambapo alieleza umeongeza situ ufanisi
bali uwazi na umechangia kupunguza rushwa kwani kila fedha inayo ingia
inaonekana kwenye mfumo wa kidigitali.
Aliongeza
na kusema ukuaji wa Teknolojia hii lazime uangazie pia tishio kubwa la uhalifu
mtandao ambapo lazima upatiwe suluhu ya kudumu. Wahudhuriaji wa mkutano
walionyesha kufurahishwa sana na hotuba yake hasa alipo zungumzia swala la usalama
mtandao.
Binafsi,
Nilishiriki katika mkutano huu na nikapewa heshma ya kuongoza moja mjadala
ambapo uliangazia usalama mtandao – Kimsingi dhana kuu ya mjadala nilioshiriki
ilikua situ kukumbusha kua tunapo endelea kuunganisha kila mtu na kuwekeza
zaidi katika sekta ya TEHAMA inayo endelea kuturahishia mambo mbali mbali mbali
pia unaongeza kasi ya uhalifu katika
mitandao. Aidha, mjadala pia uli jikita katika kutoa ushauri wa nini
kifanyike.
Nikizungumza
nilitolea mfano vyombo vya usafirishaji
(mfano: Magari, Treni na Ndege) vinavyoweza kuangushwa kupitia uhalifu mtandao
na nikaelezea tukio la magari Milioni 1.4 aina ya JEEP yaliyo lazimika
kurudishwa kiwandani baada ya kuweza kuangushwa na wahalifu mtandao.
Aidha,
nilizungumzia tukio la mifumo ya umeme ya Nchi ya Ukrine iliyoweza kuzimwa na
wahalifu mtandao, Pesa zinazopotea kwa kasi kupitia uhalifu mtandao na taarifa
mbali mbali zinavyo endelea kuinbiwa kupitia mtandao huku tovuti na mifumbo
mbali ya kidigitali inavyo angushwa kila siku na wahalifu mtandao.
Niliendelea
na kusema pamoja na hali hii kuwa ni ya kutisha wana usalama mtandao duniani
kote tumeendelea kutafuta suluhu ya matatizo na kuendelea kushauri matafa mbali
mbali juu ya nini cha kufanya ili kuendelea kubaki salama kimtandao.
Kiujumla
mkutano ulikua ni wenye faida kubwa na tumekubaliana kufanyia kazi tuliyo
yazungumza na pia binafsi nikitegemewa ikiwa ni moja ya makubaliano kuweza
kuzuru mataifa kadhaa ili kuweza kuimarisha mashirikiano katika swala la
kukabiliana na uhalifu mtandao.
HABARI NJEMA: Tanzania kupitia Chuo cha Nelson Mandela
cha Arusha ambapo pia niliweza kukitembelea hivi karibuni kipo katika hatua
nzuri ya kuanzisha mafunzo ya usalma mtandao katika ngazi ya shahada ya pili
(Masters) ambapo ni katika kuhakiki kama taifa tunaendelea kukuza wataalam wetu
wa ndani – Jambo ambalo kwa muda nilikua nikiomba chuo hicho kiweze kutoa
mafumzo hayo na nimefarijika kuona Januari huwenda yakanza kama kila kitu
kitaenda sawa.
No comments:
Post a Comment