KWA UFUPI: ATM jackpotting imgonga Hodi Nchini Marekani ambapo imesababisha upotevu mkubwa wa fedha zinazo kadiriwa kuzidi kiasi cha Dola milioni moja hadi sasa.
----------
Kumekua
na aina nyingi za uhalifu mtandao unaolenga mashine za ATM ambao umekua
ukiathiri mabenki mengi maeneo mengi duniani.
Mataifa
ya Afrika yamesha kumbwa na changamoto za uhalifu katika mashine za ATM kama vile “card skimming” ambapo wahalifu
mtandao mara kadhaa wamekua wakiripotiwa kughushi kadi za ATM zilizopelekea
upotevu wa fedha kupitia mashine za ATM.
Toka
mwaka 2014, Kumeendelea kuibuka aina nyingine za uhalifu unao athiri Mashine za
ATM maeneo mbali mbali – Itakumbukwa Niliwahi kutoa taarifa inayosemaka hapa: TYUPKINYATIKISA MASHINE ZA ATM
Ilipo
gundulika chanzo cha uhalifu huo kulipelekea kutolewa maelekezo ya namana ya kujilinda
ambapo Mabenki mengi hayakuzingatia – Kitu kilichopelekea kuibuka kwa uhalifu
mwingine aina ya ATM Jackpotting, Ambapo mwaka 2015 Nchi za bara la Asia, Ulaya
na marekeani ya Kusini walikumbwa na Uhalifu aina ya Remote ATM Jackpotting (RAJ)
Maelekezo
Zaidi yalitolewa na baadhi ya Nchi zikachukulia uzito ulinzi mtandao katika
mashine za ATM ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa.
Toka
mwaka Jana ATM jackpotting imeendelea kukumba mataifa ya Marekani kusini ingawa
sio kwa kiasi kikubwa.
Na
Mwaka Huu wa 2018, ATM jackpotting ikagonga Hodi Nchini Marekani ambapo
imesababisha upotevu mkubwa wa fedha zinazo kadiriwa kuzidi kiasi cha Dola
milioni moja hadi sasa.
#Infosec #ATM Jackpotting, a way of making ATMs spit out cash without the need of a PIN, has reached the U.S - @kaspersky has reported.— YUSUPH KILEO (@YUSUPHKILEO) January 31, 2018
We have seen similar attack in 2015 affected a number of countries
No single country is immune to this type of #CyberAttack - We must get ready pic.twitter.com/HfBOuHWtTc
Natumia nafasi hii kukumbusha mabenki yetu mambo makuu ma tatu kwa sasa.
Moja,
ELIMU YA UELEWA (Awareness) – Tumehimiza elimu kubwa ya uelewa ifanyike katika
taasisi za kifedha ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wafanyakazi wa taasisi hizo
juu ya kutambua na kujilinda dhidi ya uhalifu kama Social engineering, Key
loggers, Phishing na aina nyingine zozote zinazoweza kupelekea benki husika
kukumbwa na uhalifu wa ATM Jackpotting pamoja na aina nyingine za kihalifu.
Aidha, Elimu kwa watumiaji wa Mashine na mifumo mingine ya kibenki inapaswa
kufanyika pia.
Mbili,
MIFUMO YA UFATILIAJI (Implementation of Monitoring tools) – Kampuni nyingi zinazojihusisha na
usalama mitandao zimekua zikiwekeza kwenye uzalishaji wa mifumo inayo saidia
kufuatilia na kubaini aina yoyote ya viashiria vinavyoweza kupelekea uhalifu
wowote wa kimtandao katika taasisi zetu.
Naziasa taasisi za fedha kuhakiki
zinachukua hatua za muhimu kuweka na kuimarisha mifumo iyo ili iwe ni usaidizi
wa kubaini viashiria vyovyote vya uhalifu mtandao.
Tatu,
KUONDOKANA NA MATUMIZI YA WINDOW XP KATIKA MASHINE ZA ATM – Hili tumekua
tukizungumza toka kuonekana ya kua uhalifu wa Tyupkin uliathiri Zaidi mashine
za ATM ambazo zilikua na Window XP. Wito ni kua kuna kila sababu wa Taasisi za
kifedha kufanya operation ya haraka kuhakiki ina angazia mashine zake zote za
ATM na kuziboresha kwa kuweka mifumo iliyo juu ya window XP.
No comments:
Post a Comment