Kukabiliana
na uhalifu mtandao lazima papatikane mashirikiano "Collaboration" – Mashirikiano ya ndani
pamoja na nje. Mara baada ya Hotuba yangu Nchini Afrika kusini ambapo niliibua
dhana ya kuwekea mkazo kwenye kuimarisha ushirikiano kwani uhalifu mtandao hauna mipaka na uharibfu wake ni wa kupindukia. Mengi yameendelea
kuonekana na dhana imeendelea kubeba uzito huku mataifa mengi yakihakiki
yanazingatia hili kwa kuanzisha au kuunganisha vitengo vinavyosimamia dhana ya
ushirikiano katika kukabiliana na uhalifu mtandao Duniani Kote.
Aidha,
Bado uhalifu mtandao umeendelea kukua maeneo mbali mbali ambapo imeonekana
wahalifu mtandao wamejipanga upya na nguvu mpya – Huwenda ni baada ya Raisi wa
Marekani Kuzuia kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana kukutana. Hatua
aliyoichukua baada ya kuona mikutano yao ya kihalifu mtandao ilikua ikionyesha mafanikio kwa kukuza
uhalifu mtandao maeneo mengi duniani hasa Taifa hilo.
Tahadhari
na maangalizo mbali mbali yameendelea kutolewa ili kuruhusu makampuni ,watu
binafsi na Mataifa kujipanga zaidi na dhana ya kuzuia tatizo kabla halijatokea. Ambapo katika
hotuba yangu Nchini Kenya mwishoni mwa mwaka jana hili nililiimiza zaidi.
Kama
ilivyo ada, katika kupitia mapitio kadhaa ya kihalifu mitandao na ukuaji wa
matumizi ya TeknoHAMA tumeendelea kutoa taarifa ya mategemeo ya uhalifu mtandao
katika mwaka huu ili pia kutoa fursa ya mataifa kujipanga kukabiliana nayo
yatakapo jiri na hata kujitahidi kutengeneza njia rafiki ya kuzuia kabla
hayajatokea.
MAFANIKIO
Mapema
mwanzoni mwa mwaka huu hatimae wahusika wa uhalifu mtandao uliotikisa anga ya
usalama mtandao ambapo pesa nyingi zilifanikiwa kuingia mikononi mwa wahalifu
baada ya kufanikiwa kuingiza kirusi cha Tyupkin kwenye Mashine za kutolea fedha "ATM" na kusababisha pesa
kutoka bila mpangilio wamefanikiwa kutiwa nguvuni. Taarifa ya Tyupkin ilipojiri
niliitolea ufafanuzi kupitia andiko linalosomeka kwa “KUBOFYA HAPA”
Aidha,
Kupitia dhana ya ushirikiano baina ya mataifa mbali mbali ambapo pia imekua
chanzo cha kufanikisha upatikanaji wa wahusika wa Tyupkin, Watuhumiwa wengine
wa wili waliohusika na kundi la “DD4BC DDOS extortion” wametiwa nguvuni.
Mpango
kabambe ulipangwa kuhakiki kundi hili lililo umiza vichwa vya wanausalama
mitandao linasambaratishwa ambapo mataifa mengi yaliunganisha nguvu kukabiliana
nalo na hatimae wiki hii mwanzoni ndoto ikatimia. Inaaminika wawili waliotiwa
nguvuni si mwisho wa tatizo na bado jitihada zaidi zinaendelea.
KASI YA UHALIFU MTANDAO
Wakati
mafanikio kadhaa kutoka katika mataifa mbali mbali hasa barani Ulaya ambapo kwa
hakika tayari wamekua na mpango madhubuti baina ya Nchi zao kukabiliana na
uhalifu mtandao huku wakishirikiana kwa karibu na mataifa nje ya umoja wao
kufikia malengo bado tumeendelea kuona matukio kadha ya kihalifu mtandao ndani ya mwaka huu katika maeneo
mengi.
Nchi
ya Ukraine, Wahalifu mtandao walifanikiwa kuzima umeme ambapo tukio hilo
limetafsiria kama “Wakeup call” kwa mataifa mengine kwani tayari hili lilisha
bashiriwa kua mataifa yajipange kwenye mifumo ya umeme kwani wahalifu walisha
tengeneza mikakati ya kuidukua na kuleta madhara.
Taarifa za awali zinaeleza kua uhalifu huo chanzo kimeonekana kutokea Nchini Urusi.
Marekani imeshasema itatoa ushirikiano wa dhati kujua mzizi wa tukio husika na
ufumbuzi kupatikana. Wakati Marekani ikijipanga kutoa usaidizi kwenye hili-
onyo limetoka kua huwenda nayo ikawa nchi itakayofatia kwenye uhalifu huu hivyo
nayo ijiweke/ijipange vizuri mapema.
Nissan
nayo haijabaki salama, Wahalifu mtandao wa kundi la “Anonymous” wamefanikiwa
kuidukua na kuiangusha wakidai ni namna yao ya kuandamana dhidi ya Japan.
Nissan kufuatia tukio hilo ililazimika kufunga tovuti zake mara moja ikiwa ni
hatua za kuhimili vishindo vya uhalifu huu mtandao dhidi yake.
#infosec - Update on @Nissan #Cyberattacks : It shuts down websites after anti-whaling cyber attack @zainabchondo @bbcswahili
— YUSUPH KILEO (@YUSUPHKILEO) January 13, 2016
Swala
la Makampuni ya magari kudukuliwa sio geni na mwaka jana tulishuhudia magari aina ya "Jeep" kuingiliwa na wahalifu mtandao yaliyosababisha magari hayo kupata ajali
zisizotegemewa baada ya wahalifu mtandao wakiwa mbali kuweza kuyasababishia
ajali hizo.
Nigeria pia Hamkani si shwari , Jumatatu
ya wikii hii, Wakati ufunguzi wa mafunzo maalum ya kiuslama mtandao – Waziri wa TEHAMA wa Nchi hiyo Mh. Adebayo Shittu aliainisha kupitia
hutuba yake kua makundi ya kihalifu mtandao yameendelea kulitesa taifa hilo kwa
kuathiri wizara, mashirika ya kiserikali, mashirika ya kifedha na penginepo
ambapo uhalifu huo umeendelea kuigharimu nchi hiyo zaidi ya dola za kimarekani Milioni 400 kila mwaka.
Mafunzo
hayo maalum ni katika utekelezaji wa azimio la kuongezea uwezo wataalam tulio
nao – Azimio ambalo limeendelea kutekelezwa na mataifa kadhaa kitaifa. Binafsi
nategemewa kuendelea kushiriki kwenye mpango huu kwa Nchi ya Kenya kufuatia mwaliko maalum. Nitumie fursa hii kutoa wito kwa taifa la
Tanzania kuliangazia hili kwani ni moja ya njia sahihi za kukabiliana na
uhalifu mtandao nchini.
Marekani nako wahalifu wame chachamaa, Nchi hiyo imetoa tamko kua kufuatia uangalizi kwenye
mitandao yake, imebaini wahalifu mtandao waki vamia zaidi mifumo ya makampuni
yao na tayari wameaza kuimarisha namna ya kukabiliana na uvamizi huo huku
ikitahadharisha kuonekana kwa uhalifu mtandao kutegemewa kutatikisa zaidi mataifa mengi mwaka
huu.
ANGALIZO - TAHADHARI
Microsoft
imetangaza kwamba imeacha kutoa usaidizi wa kiufundi kwa matoleo ya awali ya
kisakuzi chake cha Internet Explorer na kuwaweka hatarini mamilioni ya watu
wanaotumia matoleo hayo.
Mabadiliko
hayo yataathiri matoleo nambari 8, 9 na 10 ya kisakuzi hicho.
Baadhi
ya mashirika yanakadiria kwamba matoleo hayo hutumiwa na takribani asilimia 20
ya Computerworld inasema kati ya watu wanaotumia Internet Explorer, ni asilimia
55 pekee wanatumia matoleo ya majuzi zaidi.
Visakuzi
hulengwa na wadukuzi na wataalamu hubashiri uwezekano wa mashambulio kutokea na
kuweka kinga kupitia kutoa matoleo mapya.
"Kuanzia
Januari 12, 2016, ni toleo la karibuni zaidi la Internet Explorer litapokea
usaidizi wa kiufundi na maboresho ya kiusalama,” Microsoft wamesema.
"Microsoft
inawahimiza wateja kuboresha na kutumia toleo la majuzi zaidi na ili kuchakura
mtandaoni kwa njia salama zaidi.”
Kampuni
hiyo inaendelea kutoa usaidizi kwa matoleo ya IE 11 na Edge, ambayo kimsingi
ndiyo hutumiwa na Windows 10.
NetMarketShare
inakadiria kwamba wanaotumia Internet Explorer mtandaoni ni 57% wakilinganishwa
na 25% wanaotumia Chrome, 12% wanaotumia Firefox na 5% wanaotumia Safari.
Aidha,
Uhalifu unao sababisha kufunga kwa mfumo
wa mtumiaji na kumtaka atoe kiasi cha pesa ili aweze kuendelea na huduma maarufu
kama “Ramsomware” unashika kasi hivyo makampuni na watu binafsi hawanabudi
kujipanga.
MATARAJIO
2016 YA KIHALIFU MTANDAO
Watu
binafsi, Makampuni na mataifa yameaswa kujipanga zaidi kufuatia matarajio na
ongezeko la uhalifu mtandao mwaka huu ambapo zaidi tunategemea kuona na baadhi
tayari yameanza kuonekana uhalifu mtandao utatikisa zaidi maeneo yafuatayo.
Matarajio
ni kua Sekta ya Umeme, Anga na Elimu (Vyuo) vitegemee kupata itilafu ya
kiuhalifu mtandao. Bado Mabenki nayo kupitia aina tofauti kadhaa mpya za uhalifu
ili kuiba pesa ni miongoni mwa vinavyo tajwa.
Sekta
ya Umeme tayari tumeona Ukraine ikifungua dimba huku mataifa mengi yakiaswa
kujipanga. Wakati huo huo sekta ya Anga mpango kabambe wa kuimarisha kujipanga
umewekwa huku tamthilia ya “CSI Cyber” ikitoa episodi maalum kulizungumzia hili
mapema mwaka huu.
Hili
likijiri Umoja wan chi za Ulaya “EU” imeanzisha rasmi “Digital ‘SWAT’ Team for
Aviation” ambapo wataalam wabobezi watapata ajira kukabiliana na kujipanga
dhidi ya tishio hili la kihalifu katka sekta ya Anga.
Vyo
Kadhaa tayari vimeingiliwa na wahalifu mtandao na baadhi wametiwa nguvuni huku
mataifa kadhaa yakijipanga kwenye hili.
Matarajio
haya ni kwa uchache – Ila jitihada za mwaka huu maangalizo na kutumia njia
mbali mbali patakua na mpango kabambe ya kuyatolea ufafanuzi sanjari na
kuainisha namna ya kujipanga kukabiliana na hali mbaya ya kihalifu mtandao.
Nichukue Fursa hii tena kutoa wito kwa taifa la Tanzania kua sikivu kwenye hili
ili kuweza kujipanga mapema na hali ya kihalifu mtandao kabla ya mambo
kuharibika na kuanza kukimbizana kutafuta suluhu ya changamoto.
No comments:
Post a Comment