Ikiwa
bado Singapore inaendelea na mkakati wake wa kua “Smart Nation” imeanisha
kuweza kufikia hapo lazima swala la usalama mitandao liwe muhimu zaidi “Top
priority”. Hii ni kutokana na uhalisia kua Nchi inapokua ya kisasa zaidi na
kutumia kwa wingi mifumo yaki Teknohama katika maeneo mbali mbali uhalifu
mtandao nao unaongezeka.
Mwaka
jana (2015) katika kuliendea hili la kuhakiki Usalama mtandao unashika nafasi
ya juu kwa taifa hilo linalokua kwa kasi barani Asia, Wali anzisha wakala wa
usalama mtandao “Cybersecurity Agency” ambapo uliiunganisha vitengo vyote
vidogo vya usalama mitandao na kukuza ushirikiano na sekta binafsi nchini humo.
Hatua
hiyo ilipongezwa na wana usalama mitandao Duniani kote na binafsi kuliandikia
katika andiko linalosomeka “KWA KUBOFYA HAPA”. Tayari nchi hiyo pia ina mpango
wa kimkakati wa miaka mitano wa kitaifa wa usalama mtandao “National
Cybersecurity Master plan” ambapo inategemewa kuwekeza zaidi katika kulinda
miundo mbinu yake ya TEHAMA pamoja na taarifa zake pamoja na Wananchi wake.
Nchi
hiyo ya Singapore haikukomea hapo tayari imesha boresha mashirikiano yake na
Nchi nyingine za barani Asia ambapo makubaliano maalum kwa nchi hiyo
(Singapore), Japan, India na Malaysia ya kuimarisha zaidi ushirikiano ya kimkakati yameshawekwa
mapema mwaka huu (2016) ili kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao.
Nguvu
hii ya pamoja ya kushirikiana kukabiliana na uhalifu mtandao ni hatua ya Muhimu
kwa Nchi hizo za barani Asia – Tayari hadi sasa tumeshuhudia mafanikio mengi
kwa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) kutokana na hatua za kuunganisha nguvu katika
mashirikiano ya pamoja na ya dhati kukabiliana na uhalifu Mtandao.
Kampuni
ya Usalama mitandao ya FireEye, Imeainisha Nchi hiyo kua na uwezo mkubwa zaidi
barani Asia kukabiliana na uhalifu mtandao. Ingawa bado Nchi hiyo aliiaswa na
kampuni hiyo kufunga mkanda zaidi kwani Wimbi kubwa la uhalifu mtandao bado
limeendelea kuzitesa Nchi zenye uwezo mkubwa wa kiulinzi mtandao na kuitolea
mfano Nchi ya Marekani.
Katika
taarifa ya FireEye, Inaeleza Wahalifu Mtandao wameendelea kuitesa Marekani na
kuifanya Nchi hiyo kuendelea kuongeza nguvu zaidi kukabiliana na wimbi kubwa
uhalifu mtandao. Hivyo Nchi ya Singapore lazima Iendeleze jitihada zaidi kuendelea
kuimarisha usalama mtandao wa Taifa hilo.
Ikumbukwe
mataifa sasa yame imarisha zaidi si tu mifumo yao ya usalama mitandao bali hata
majeshi ya kiusalama mitandao ambayo yameendelea kutumika kuibia mataifa mengine
taarifa muhimu na kukabiliana na aina yoyote ya vita mtandao.
Tulipofikia
sasa Mataifa mengi yamekua hayapeleki watu wake kwenye Nchi nyingine kwa nia ya
kupata taarifa mbali mbali ambazo ni muhimu na badala yake wameendelea
kujiimarisha kwenye njia mbali mbali za ki TEHAMA zinazo weza kufanikisha hili pasi
na kumueka yeyote kwenye hatari ya kukamatwa katika Nchi ya Kigeni.
Tumeshuhudia
hili kwa mataifa kama China, Marekani, Urusi, Korea na kwenginepo. Hadi sasa
mataifa Takriban 50 yana nguvu za kihalifu mtandao za kitaifa “offensive cyber
capabilities”. Wataalam wa usalama mitandao tumeendelea kusisitiza kua na nguvu
hii na kuweza kudhuru Nchi nyingine kimtandao “Cyber Espionage” ina uwiano sawa
na ugaidi mtandao.
Hadi
sasa Katika mataifa hayo 50 yaliyo jiimarisha ki nguvu mtandao kuweza kudhuru
mataifa mengine Singapore si miongoni mwao – Mkurugenzi wa TEHAMA wa Kampuni ya kiusalama mtandao ya
“DarkTrace” imelishauri taifa hilo
(Singapore) kujipanga kwenye hilo na kuhakiki imekua na Jeshi mtandao ili kuweza
kukabiliana na taifa lolote litakalo weza kuhitaji kudhuru taifa hilo kimtandao.
Hii
ni kutokana na Mikakakati yake pamoja na
ukuwaji wa taifa hilo kwa kasi huwenda mbeleni Baadhi ya mataifa yakawa na
dhamira ya kuidhuru Nchi hiyo kimtandao. Marekani kwenye Taarifa inayosomeka
“KWA KUBOFYA HAPA” ime eleza wazi iko tayari kivita Mtandao na Nchi Yoyote.
Na Kwa Mara ya kwanza katika historia ya udukuzi, Kampuni ya Kichina ambayo kwa muda mrefu wahalifu mtandao wamekua wakitaka sana kufanikisha kuidukua bila mafanikio mwaka huu imewezekana. Taarifa zaidi zinasomeka kwa "KUBOFYA HAPA" Hili pamoja na tukio la wahalifu mtandao kudukua mifumo ya umeme ya Ukraine na kufanikisha kuzima umeme na kusababisha usumbufu na uharibifu mkubwa yametafsiriwa na wana usalama mtando kua wahalifu mtandao wanazidi kuongeza makali kufanikisha uhalifu mtandao maeneo mengi duniani.
TANZANIA: NINI TUNAJIFUNZA?
Ikumbukwe
Serikali ya awamu ya Nne (4) ya Dr. Jakaya kikwete iliwekeza sana kwenye
kuimarisha miundo mbinu ya KITEHAMA – Tukaweza kuwa na Mkonge wa Taifa, Ghala
la kuhifadia taarifa la Taifa “Natinal Data Center” pamoja na kuchukua taarifa
za wana nchi kwenye usajili wa Vitambulisho vya Taifa pamoja na kupigia kura
ambapo taarifa hizi muhimu za wananchi wa Tanzania zimehifadhiwa kwenye mifumo
ya KiteknoHAMA.
Hayo
pamoja na mengine mengi tuliyo shudia na yanayoendelea kuwekewa mikakati ili
kuhakiki Taifa la Tanzania linaendelea kujikita zaidi na matumizi ya TEHAMA
maeneo mbali mbali yana liweka taifa pia katika hatari ya kuweza kdhuriwa zaidi
na Uhalifu Mtandao.
Lazima
Taifa kama Taifa liangazie macho swala hili muhimu la usalama mitandao kama kwa
umakini wa kipekee ili kuhakiki Maeneo mbali mbali yatakayo tumia mifumo ya
TEHAMA yanabaki salama kimtandao.
Wizi
wa Taarifa na fedha zinazopotea kupitia Uhalifu Mtandao unaweka taifa lolote
katika hali mbaya na kusababisha kuyumbisha Uchumi, Siasa na Nyanja nyingine
mbali mbali.
2014,
Wakati Mataifa takriban 21 yalipokutana Nchi kujadili maswala ya usalama
mitandao, Mengi yalizungumzwa na kuonekana kua hatuna budi ila kuhakiki swala
la usalama mtandao linawekewa mkazo. Kwa Ufupi Yaliyosema na kujiri kwenye hilo
yanaweza kutazamwa kwnye Video inayo weza kutazamwa kwa “KUBOFYA HAPA”
Nimepitia
Moja ya Andiko pamoja na Michango mbali mbali iliyotolowa ambapo linaweza
kusomeka kwa “KUBOFYA HAPA” ambapo nimeona kuna mambo kadhaa ambayo bado Ni
CHANGAMOTO kwetu kama ifatavyo: -
MOSI,
Vitengo vya TEHAMA kwa Ujumla vimeonekana kuwa na uwezo mdogo wa kuweza kufanya
kazi yake ipasavyo. Mfano:
Yalitolewa maelekezo hivi karibuni na Ofisi ya Raisi ya kuwapo na Vitengo vya
huduma kwa wateja katika ofisi na mashirika ya serikali. Kitu ambacho Vitengo
vya TEHAMA Nchini vingeweza kua na mwanzo (Bila Gharama yoyote) kwa kuwa na mifumo
ya kutumia Mitandao ya kijamii kusikiliza shida mbali mbali za wana Nchi
kupitia kurasa rasmi zitakazotoa fursa kwa wananchi kueleza waliyo nayo ili
kupatiwa utatuzi.
PILI,
Kumeonekana kua na changamoto ya kuwako na wenye uwezo mdogo wa kugeuza
changamoto kuwa fursa KITEHAMA ili kufikiwa kwa malengo mbali mbali. Mfano: Wakuu wa TEHAMA wamekua
wakionekana kuhofia sana kushirikiana / Kushikisha wataalam wa Ndani kuwasaidia
mawazo ya kutatua mambo mbali mbali kitu ambacho mara nyingi husababishwa na
Uwezo mdogo wa muhusika na kuhofia sana kuweonekana mapungufu.
TATU,
Kumekua na kufanikiwa kutokea kwa uhalifu mtandao Nchini na bahati mbaya zaidi
wakati mwingine unadumu bila hatua zozote kuchukuliwa. Mfano: Nilipata kueleza mwanzo kulibashiriwa na wana usalama
mitandao kua uhalifu wa “Click Jacking” ungeikumba Tanzania, Uhalifu huo
hatimae ulilikumba taifa kutokana na kudumu kwa muda kutokana na kushindikana
kua na mpango wa kimkakati kukabiliana na hili mapema kabla hata ya kuathiri
taifa.
Hayo
ni kwa uchache ingawa Changamoto ni nyingi zaidi ambazo zipo na zina hitaji
utatuzi. Katika Hotuba yangu kwa niaba ya Nchi za Afrika Nchini Afrika Kusini
ambapo wana usalama Mtandao kutoka mataifa mbali mbali tulikutana pamoja
kujadili changamoto na nini kifanyike niliainisha njia rafiki na madhubuti za kufanyiwa
kazi ili kupiga hatua katika kuimarisha usalama mitandao.
Hotuba
hiyo iliyo ungwa mkono na Wote akiwemo Mkuu wa Wakala wa Usalama wa Nchi ya
marekani (NSA) aliyemaliza muda wake na wengine baadae maazimio yaliendelea
kufanyiwa kazi na mataifa mengine mbali mbali na tayari matunda ya kuridhisha
yameendelea kuonekana.
Nilitolea
ufafanuzi kwenye hutuba hiyo na mengineyo yaliyo jiri katika Video hapo Chini
ambapo naimani kabisa endapo Taifa la Tanzania lika amua kufanyia kazi basi
tutapiga hatua kubwa sana ukizingatia sasa Raisi wa awamu ya Tano, Dr. J P
Magufuli ameonyesha dhamira ya dhati ya kuimarisha uchumi wa Taifa letu –
Uchumi ambao Kupitia Uhalifu Mtandao unaweza kuyumbishwa na wahalifu mtandao
kupitia namna mbali mbali.
KWAKUANZIA, Tuanze na Kufanyia kazi “Right Skillset to the Right Places” tutumie wenye
uwezo kwenye maeneo stahiki. Kisha tuendelee kuwaongezea ujuzi wataalam wa
ndani kuendana na mabadiliko ya kasi katika Teknolojia “Capacity building” Bila kusahau
kuimarisha elimu ya uelewa “Cybersecurity Awareness program” Pamoja na
kuimarisha mashirikiano ya ndani “Collaboration”. Bahati Nzuri Sheria Mtandao “Cyber Law”
Imepaikana na inafanya Vizuri.
No comments:
Post a Comment