WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Monday, 29 February 2016

UHALIFU MTANDAO NA ELIMU YA UELEWA (AWARENESS)

Uhalifu mtandao umeendelea kua changamoto maeneo mengi Duniani.Taasisi za kifedha, Usafirishaji, Nishati,na maeneo mengine mengi yameendelea kukabiliwa na matukio ya kihalifu mtandao huku athari zake kuendea kukua kila kukicha.

-------------------
NEWS UPDATES: Following a pair of breaches, LINODE is now changing user procedures to improve security. The web hosting company was the target of two breaches over the past year. Both incidents, one in July 2015, the other in December 2015, involved stolen customer account access credentials. In response to the December  breach, Linode force-reset all customer passwords. The company is changing authentication procedures to separate customer application from credentials. Linode is also employing credit card tokenization, and altering its internal policies with guidance from a NIST framework.
-------------------

Mataifa mengi yameendelea kuwekeza kwenye Vitendea kazi (Vizuizi - Tools), Kuimarisha ushirikiano ndani na kuvuka mipaka ya Nchi (Collaboration) kuongezea elemu wataalam wa kukabiliana na uhalifu mtandao (Capacity building) huku sheria za uhalifu mitandao zikionekana kuboreshwa zaidi kwenye mataifa mengi. Yote haya yakiwa ni hatua za kukabiliana na uhalifu mtandao.

Ifahamike, Elimu ya uelewa ndio SILAHA kuu – Mataifa mengi bado Imekua ni Nadra kuona mikakati Madhubuti ya elimu ya uelewa (Awareness) stahiki na endelevu itakayo mpa fursa Mwananchi wa kawaida kuweza kujikinga binafsi na kufahamu namna ataweza kutatua tatizo pale atakapo kabiliwa na uhalifu mtandao.


Kulitambua hili Katika kukabiliana na uhalifu mtandao jambo la kwanza limekua ni kuhamasisha elimu ya uelewa. Na katika maazimio 11 ya mwaka jana Elimu ya uelewa ilikua ni azimio la kwanza. Aidha, Wataalam wa usalama mitandao wameendelea kutengeneza Video, Katuni, Michezo na mengineyo yenye malengo ya kukuza uelewa kwa jamii juu ya matumizi salama ya mifumo yetu ya Ki TEHAMA.

Pamoja na jitihada hizi na kupatikana mwezi maalum wa kukuza uelewa (Octoba) bado pameonekana changamoto kadhaa zinaz sababisha elimu hii ya uelewa kutotoa matunda tunayotegema.

Mosi, Elimu ya uelewa imekua si endelevu – Unaweza kukuta shirika/Kampuni na hata Taifa linakua na elimu ya uelewa kwa wakati Fulani na baadae kusahaulika kabisa. Na maeneo mengi unakuta Mwezi Octoba pekee ndio elimu ya uelewa inatolewa zaidi huku miezi mingine pakiwa hakuna elimu hii.

Nini Kifanyike, Elimu ya Uelewa lazima iwekewe taratibu maalum Walau kila baada ya miezi mitatu na ikiwezekana Katika Vikao vya asubuhi Makazini Kwa Wiki Mara Moja kutolewe elimu hii.

Pili, Elimu ya uelewa kukosa ubora – Kutokana na Msisitizo ambao upo wa kuhakiki elimu ya uelewa inatolewa, wanao tekeleza hili wamekua hawafati Maelekezo sahihi ya namna ya kufikisha elemu hii kitu kinachopelekea kuona elimu hii kuwepo bila mafanikio kuonekana.

Nini Kifanyike, Kama ilivyo katika mambo mengine – Elimu ya uelewa ina taratibu zake za namna ya kuifikisha kwa walengwa ili kuweza kuonyesha matokeo tegemewa. Ni lazima taratibu hizi ambazo tumekubaliana kimsingi baina ya wataalam kote duniani kufatwa ili kuhakiki elimu husika inakua na ubora stahiki na tunafikia malengo tegemewa.

TANZANIA: Moja ya mambo kadhaa ambayo nimekutana nayo ninapo shiriki katika mijadala au niwasikilizapo wadau/wanachi wanapo zungumzia swala la usalam mtandao – Kilio Kikuu imekua ni kukosekana elimu ya uelewa. Mfano Ni mjadala Unaoweza kusomeka kwa “KUBOFYAHAPA”

Ki Uhalisia elimu kwa kiasi chake imekua ikitolewa lakini haifikii Malengo tarajiwa kutokana na kutokidhi vigezo – Imekua ikitolewa kimazoea tu bila kufata taratibu stahiki ambazo zimekubaliwa kimsingi na wataala wote kutoka maeneo yote duniani. Na Hili ndio tatizo kubwa. Hatuna budi kubadilika.

Elimu ya uelewa inapotolewa ipasavyo na ikaonyesha matunda tegemewa ina uwezo mkubwa wa kupunguza uhalifu mtandao Nchini kwa takriban Asilimia 75%.

Nilipata andikia makala Ndefu yenye ufafanuzi wa Njia Madhubuti ya kukabiliana na uhalifu mtandao inayoweza kusomeka kwa “KUBOFYA HAPA” ambapo nilianisha mambo mengi ya kuzingatiwa na umuhimu wa elimu hii kwa jamii zetu.


Natoa Wito – Elimu hii ya Uelewa iweze kupewa kipaumbele stahiki ikiwa ni silaha tosha ya kukabiliana na uhalifu mtandao Nchini ambao unaonekana kutaka kuanza kushika Mizizi.


When was Your Last time you updated your Password? - Lini Ilikua mara yako ya Mwisho kubadili neno lako la siri?

No comments:

Post a Comment