Matukio
yaki halifu mtandao kwa mwaka huu wa 2016 yameonekeana kushika kasi zaidi ya
ilivyotegemewa. Tayari kumekua na matukio kadhaa ya kihalifu mtandao ambapo
baadhi yao watoto wa umri kati ya miaka Tisa (9) na Kumi na saba (17)
wanahusika.
Hali
hii pamoja na tishio la makundi ya kihalifu mtandao kutishia kuyumbisha UCHUMI
wa mataifa mengi duniani imepelekea wana usalama mtandao kuzidi komba mataifa
mbali mbali kujipanga zaidi kukabiliana na uhalifu mtandao.
Mapema
Mwezi huu, taarifa binafsi za wanavyuo wa chuo cha Greenwich zimeonekana
kusambazwa mitandaoni. Kufuatia mamia ya
taarifa za wanachuo hao kupatikana mtandaoni, Chuo hicho kimeomba radhi na
tayari chuo hicho kinaendelea kuwasiliana na wanachuo wote walio athirika na
tukio hili. Wakati huo huo tukio hilo limeripotiwa na upelelezi bado
unaendelea.
Uchunguzi
wa awali umeonyesha huwenda wadukuzi walifanikiwa kuingilia mifumo ya chuo
hicho na kusababisha taarifa hizo binafsi kusambaa mitandaoni. Tukio hili
linafatia tukio la kijana wa miaka 16 kudukua mifumo ya vyombo vya usalama
Nchini marekani pamoja na barua pepe ya mkurugenzi wa CIA ambapo taarifa
zilizopatikana huko pia zili anikwa mitandaoni.
Wanasheria
wameonya tukio hilo linaweza kuligharimu chuo hicho pesa nyingi endapo wana
vyuo hao watashitaki kutokana na taarifa zao binafsi walizo zipatia chuo hicho
hazikupatiwa ulinzi wa kutosha na hatimae kuishia mikononi mwa wahalifu
mtandao.
Miongoni
mwa taarifa za wanachuo zilizopatikana mitandaoni ni pamoja na majina yao,
Namba zao za simu, Miaka yao ya kuzaliwa, Mahli wanapo ishi, Sahihi zao,
taarifa zao za hospitali (medical history) pamoja na mambo mengine.
Kwa
sasa Taarifa hizo zime ondolewa mtandaoni na chuo hicho kimesha fanya
mawasiliano na Google kuhakiki taarifa hizo haziendelei kuonekana kupitia
kisakuzi cha google.
----------------------------------------------------------
NEWS UPDATES: Computer systems at the Hollywood Presbyterian
Medical Center in southern California have fallen prey to ransomware. The
systems have been offline for more than a week. Employees were not able to
access patient files and the hospital declared the situation an internal
emergency. The FBI, the Los Angeles Police Department, and cyberforensics
experts are investigating. The attackers have demanded a ransom of 9,000
Bitcoins (approximately US $3.6 million; 3.2 million euros.)
--------------------------------------------------------------
Aidha,
Ripoti iliyokua ikingojwa ya “Horizon scan” iliyokua ikiandaliwa na taasisi ya
maendeleo ya biashara, BSI imetoka. Ripoti hiyo iliyo fanywa kwa kukusanya
maoni kutoka kwa mashirika makubwa kujua hofu yao kubwa inayo ikumba makampuni
ni ipi kwa mwaka huu wa 2016 imeonyesha makapuni mengi yanahofu na uhalifu
mtandao ambapo wanaamini kuna uwezekano mkubwa uhalifu huu kuyumbisha ukuaji na
kuendelea kwa makampni mbali mbali.
Imeainisha
makampuni yameendelea kuingiwa na hasara mara kwa mara baada ya wahalifu
mtandao kufanikiwa kuiba fedha nyingi na kusababisa kuyumba kwa ukuaji wa
mapato.
Kwa
miaka miwili mfululizo uhalifu mtandao kuonekana kushika nafasi ya kwanza
katika ripoti ya taasisi hiyo.
---------------------------------------
QUOTE: A total of 48% of respondents said they were
“extremely concerned” this year about the possible threat of a cyberattack
impacting their company, such as a malware or denial of service incident.
Second on the list of top threats this year was a data breach, with 41% of
respondents saying they were “extremely concerned.” Unplanned IT and telecom
outages came in third, with 35% saying they were extremely concerned about the
threat.
-----------------------------------------
Aidha,
Kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA kunapopelekea ukuaji wa uhalifu mtandao
duniani kote kumepelekea mataifa mengi kua na mikakati madhubuti kukabiliana na
hatari ya wahalifu mtandao kuleta athari katika Nyanja zote hasa kiuchumi.
Kufuatia
hili Nchi ya Marekani kwa mara ya kwanza ameweza kuwasilisha bajeti ya Dola Bilioni
19 za kimarekani ili kukabiliana na tishio kubwa la uhalifu mtandao huku
ikiimarisha azimio la ushirikiano wa vitengo vinavyohusika na kupambana na
uhalifu mtandao nchini humo.
No comments:
Post a Comment