Mwezi
huu wa Oktoba mataifa mbali mbali yamekua yakiadhimisha kwa kukuza ufuhahamu
kwa watu wake juu yamatumizi salama ya mitandao. Ni wazi ya kuwa mitandao
inapotumika vibaya inaweza kuleta athari kubwa sana kwa jamii, na tayari
matukio mengi kutoka maeneo mbali mbali tayari tumeendelea kuya shududia.
KATIKA MWEZI HUU:
kwa uchache kabisa nitaangazia matukio baadhi nikianzia na kutokea nchini
"MAREKANI" Raisi wa Marekani Alipitisha agizo muhimu kwa taifa hilo kuhusiana
na matumizi ya kadi ili kufanyia miamala ya kibiashara ikiwa ni katika
kukabiliana na matukio ya hivi karibuni nchini mwake.tukio ambalo limeibua
mijadala mbali mbali huku mataifa mengine yakiaswa kulifanyia kazi na kuboresha
baada ya uchambuzi wa tukio hilo kufanywa na wataalam mbali mbali wa maswala ya
usalama mitandao.
"KENYA" kupitia mkutano wake mkuu wa mwaka unao wakutanisha wataalam na wafanya maamuzi
katika maswala ya TEHAMA walipata kuangalia kwa karibu maswala mbali mbali ya
kiusalama mitandao kwa kina na kuyatafutia ufumbuzi.
"TANZANIA" pia kupitia Warsha iliyofanyika na kushirikisha mataifa mbali mbali
iliyofanyikia Tume ya Taifa Sayansi COSTECH mjadala wa kina ulio jikita kwenye
maswala ya usalama mitandao ulioibua mazuri mengi ikiwa ni pamoja na kuendeleza
ushirikiano baina ya washiriki pamoja na kubadilishana ujuzi na taarifa za
msingi katika maswala ya usalama mitandao.
"CERT - EU" inayosimamia mwaswala ya usalama mitandao katika nchi wanachama za bara ulaya
walianza rasmi kujumuisha taarifa
zinazopatikana hapa kwenye tovuti yao huku mijadala mbali mbali ya kiusalama
mitandao kupitia foramu mbali mbali yakijadili taarifa zinazopatikana hapa.
"BBC - SWAHILI" na Vyombo vingine vya Habari Nchini vilionekana kuhamasisha matumizi salama ya
mitandao, hatua ambayo naipongeza sana – Hii ni kwa sababu , vyombo vya habari
vimekua na nafasi kubwa sana katika kuhakikisha wananchi wanapata ufahamu mzuri
wa matumizi salama ya mitandao ili kuweza kujiweka salama wao na taifa lao kwa
ujumla.