Mwaka
2014 Umekua Wenye changamoto nyingi sana kwenye upade wa mitandao ambapo
wahalifu mtandao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuitikisa anga ya usalama
mitandao duniani kote ambapo walifikia kutamba kuwa wameshinda mapambano na
wanausalama mitandao.
Kubwa
zaidi ni uelewa mdogo wa watumiaji mtandao juu ya kujiweka salama kimtandao
iliyo ambatana na wana usalama mitandao kuwa wachache sana katika ngazi ya
kidunia huku baadhi ya mataifa kutotoa kipaumbele katika maswala ya usalama
mitandao.
Aidha,
Mengi katika jitihada yameweza kufikiwa ikiwa ni pamoja na Kikao cha funga
mwaka cha tathmini ya hali ilivyokuwa kwa mwaka 2014 ambapo iliweza kutabiri hali
ya uhalifu mwaka 2015 na kuweka mikakati ya dhati ya kukabiliana na hali hiyo
kwa mwaka 2015 inayotegemewa kuwa na matokeo chanya. Kwenye hili unaweza
kulisoma kwenye “TAARIFA FUPI INAYOSOMEKA HAPA"
Wamarekani
nao kupitia “US department of Justice” wameamua kuazisha kitengo maalum
kitakachotoa msaada kwa mataifa yote duniani katika upande wa maswala ya
usalama mitandao ikisisitiza itaangazia zaidi katika kuzuia matatizo kabla
hayajatokea.
Tanzania
nayo haikubaki nyumba kwenye hili, Tumeshuhudia warsha, semina, kongamano na
mikutano mingine yenye malengo thabiti ya kukuza na kuongezea uwezo wa uelewa
wa matumizi salama ya mitandao paoja kukuza uwezo wa kukabiliana na hali ya
uhalifu mtandao nchini.