Mahakama
katika nchi mbalimblai zimekua na taratibu zakukusanya vielelezo vya kidigitali
vitakavyo weza toa uthibitisho katika makosa mbali mbali ya kimtandao.
Mtandano wa kijamii
wa Facebook ulitakiwa kuwasilisha taarifa za wateja wake ambao walihusishwa na
uhalifu mtandao wa kujipatia pesa kinyume na sharia kupitia mtandao wa kijamii
wa facebook.
Mtandao
huo wa kijamii wa Facebook umekata rufaa dhidi ya amri hiyo ya mahakama ambapo ilitakiwa
kuwasilisha taarifa za watu takriban 400
waliouhusika na visa vya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
Mtandao
huo wa kijamii ulisema kuwa ombi hilo la mahakama lilihusisha idadi kubwa ya
majina ya watu kuwahi kuombwa na shirika la kiserikali kutoka kwa mtandao huo
Picha
na ujumbe wa faragha pamoja na taarifa nyinginezo kuhusu watu hao
ziliwasilishwa kwenye mahakama mwaka jana, lakini mahakama ilitoa tangazo hili
wiki hii.
Uamuzi
wa mahakama ulitaja Facebook kama mhifadhi wa data za kidijitali.
Jaji
wa kesi hiyo alisema maana ya kuwa mhifadhi ni kwamba Facebook inapaswa kutii
agizo la mahakama la kutaka kufanysa msako.
Kesi
halisi ilichunguza visa vya watu kadhaa kudai malipo kutoka kwa mfuko wa taifa
kwa watu wenye ulemavu Marekani.